Tuesday, 5 January 2016
Monday, 4 January 2016
UKIONA IVI UJUE HIZI NI DALILI ZAKUCHOKWA
Saturday, 2 January 2016
NAWATAKIA WATU WOTE HERI YA MWAKA MPYA 2016
Mwaka umeanza kusonga mbele na leo ni siku ya pili Tangu mwaka uanze, Namshukuru Mungu kwakunijalia Uhai na Afya Njema na kunipa Nafasi yaupendeleo kuwepo Tena katika Mwaka huu.Mungu ni Mwema sana pia Mungu nimuaminifu kwa kila Mtu aenendaye katika njia iliyo sahihi.
Ndugu zangu wapendwa najua kila mmoja wetu anafurahi kuuona mwaka huu 2016. Lakini kuuona tu haitoshi bali tuwe na malengo na huu mwaka kama ni mwanafunzi jitahidi kusoma kwa bidii kusudi mwisho wa huu mwaka alama zako zipande zaidi ya mwaka uliopita, kama ni mfanyakazi jitahidi kufanya kazi kwa bidii nakufikia malengo yako uliyojiwekea pia kama wewe ni mkulima au mjasiriamali jitahidi katika shughuli yako kwa sababu Mungu hubariki kila kazi halali ambayo mtu huifanya kwa nguvu na akili zake.
Thursday, 6 August 2015
HIZI NDIO MBINU ZA KUTIMIZA NDOTO ZAKO
1. Fanya Kile Ukipendacho
Kuna mambo mengi hapa duniani ambayo ungeweza kuyafanya; kuna na mengine mengi zaidi ambayo ungeweza kujifunza na hatimaye kuyamudu kuyafanya. Kwa ufupi, una uwezo wa kufanya jambo lolote utakalo, endapo utajiamini na kuweka juhudi katika kutimiza jambo hilo.
Lakini sio kila jambo litakufaa wewe. Sio kila kazi utafurahia kuifanya. Sio kila kitu utakifurahia kukigusa. Kwa kuwa uwezo unao wa kufanya lolote utakalo, na kufanikiwa; hauna budi kuchagua jambo linalo furahisha moyo wako. Jambo litakalo kufanya uhisi kuwa unatoa mchango wa muhimu katika ulimwengu huu.
2. Weka Kipaumbele Katika Mahitaji ya Wengine
Hakuna kazi inayo faa, inayo pendeza, inayo furahisha na kuhamasisha kama kazi ya kutatua matatizo auhitlafu za watu wengine. Sio tu inakufanya wewe uwe mtu wa thamani katika maisha ya wengine, bali piainakupa fursa ya kupata kipato kutokana na juhudi hizo. Haijalishi ni jambo gani unalo lifanya, ilimradi linawasaidia wengine, lina faa sana.
Kuna kitu kimoja ambacho watu wote wenye kuwajali wengine wanafanania, UTAJIRI. Sio lazima uonekanokwa mfano wa mali nyingi; unaweza pia kuonekana katika uhusiano wako na watu wengine na kwa namna wengine wanavyo kuheshimu na kukuthamini. Dunia ina tawaliwa na watu wenye kuangalia mahitaji ya wengine kuliko yao, kuwa mmoja wapo.
3. Weka Bidii Kila Siku
Ghorofa halijengwi kwa siku moja, wala mafanikio kupatikana katika usiku mmoja. Usikate tamaa pale juhudi zako zinapo shindwa kuonekana na watu wengine, au msaada wako unapo shindwa kuthaminiwa na jamii. Badala yake, chukulia hii kama nafasi ya pekee ya kuboresha na kuongeza thamani ya kileunacho kifanya.
Kile unacho kifanya, kifanye kila siku. Unapo kifanya kila siku ndivyo kinavyo ongezeka thamani, ndivyokinavyo zidi kuwa chenye ubora, ndivyo watu wengi wanavyo zidi kukiona na kukijua na kukithamini. Unapofanya leo na kuacha kesho, hatimaye kukirudia kesho kutwa, kinapoteza ubora wake na kasi ya kufikia mafanikio unayo yakusudia.
4. Epuka Anasa Zisizo za Msingi
Sio kila hisia ni nzuri. Kicheko ni hisia nzuri lakini hasira ni hisia mbaya. Upendo ni hisia nzuri lakini chuki ni hisia mbaya. Vivyo hivyo katika swala la anasa au starehe. Kamwe, furaha yako usi-iegemeza kwenye starehe. Kama huna furaha na amani usitegemee utaikuta kwenye ulevi, uzinzi au madawa ya kulevya.
Furaha na amani ya kweli inapatikana katika mambo madogo-madogo yanayo tuzunguka kila siku. Kusaidiana, kushauriana, kutiana moyo, kutaniana, kucheza, kufanya kazi tunazo zipenda, kuimba, kutimiza wajibu wetu wa kila siku, kuwatembelea watu wenye madhaifu mbalimbali, kutembelea ndugu zetu wa mbalin.k. Na hizi ndizo anasa za msingi.
5. Shirikiana na Watu Wengine
Amin amin, katika ile ndoto yako unayo tamani kuitimiza, kuna mtu naye ana ndoto kama ya kwako. Kuna mtu ana ndoto ya kukusaidia wewe kufikia ndoto yako. Kuna mtu ana uwezo wa kukushauri, tena bure, ilikukuwezesha kufikia ndoto yako. Watafute watu hawa ushirikiane nao, uongee nao, uchangamane nao;watakusaidia.
Msaada wao sio tu utakusogeza mbele katika kufikia malengo yako, bali pia utakuunganisha nao na kuwafanya kuwa watu wa familia moja; wenye kutaka maendeleo. Pia utapata fursa ya kuonyesha upendo wako kwa kuwasaidia pale wanapo kwama au kushindwa; na kwa ishara hizi, amani na upendo na mafanikioyata kuzunguka siku zote.
6. Shukuru kwa Yote
Kuna wakati wewe unataka kukomba sahani na mtu anataka kukupa sahani iliyo jaa chakula. Na kwakutokujua kilichomo kwenye ile sahani mpya utaanza kulalamika, kulaani, kulaumu, kuhuzunika na kukosa amani. Kila jambo lina wakati wake, na hakuna linalo tokea pasipo ya makusudio; amini kuwa kuna faida katika kila jambo.
Kwa sababu leo hujafanikiwa haina maana kuwa hutafanikiwa kesho. Kwa sababu leo umekosa haina maana na kesho pia utakosa. Jifunze kusema ahsante. Jifunze kuridhika na kile ulicho nacho kwa wakati huo. Jifunze kushukuru hata kwa kile kidogo ulicho kipata. Kwa sababu ni kile kidogo kimoja kinacho unda kidogo kingine na hatimaye kikubwa.
Monday, 3 August 2015
HIZI NDIO SABABU ZINAZOFANYA BAADHI YA WANAWAKE KUCHELEWA KUOLEWA AU KUTOOLEWA KABISA
Pamoja na kuwa kuna wanawake husita kuolewa, lakini jambo hili si kubwa sana kwa wanawake kama ilivyo kwa wanaume. Kwa kiasi kikubwa katika suala la kutaka kuingia ndani ya ndoa, wanawake ni wengi ambao hutaka kufunga ndoa kuliko ilivyo kwa wanaume. Hilo tunaliona wazi tokana na shamra shamra awazo nazo mwanamke wakati wa maandalizi ya shughuli za Ndoa na Harusi.
Hata hivyo, kwa wale wanawake wachache ambao husuasua kuolewa hizi ni baadhi ya sababu zinazopelekea kusuasua huko. (Izingatiwe hii ni kwawanawake ambao hawajawahi kuolewa kabisa)
Vigezo vilivyopitiliza viwango (hasa kwa muonekano)
Wanawake wengi hasa wa umri mdogo (lakini unatosha kuolewa) hutumia muda mwingi katika kuchagua aina ya mwanaume ambaye angependa awe mume wake. Wanawake hawa hujiamini zaidi na kusimamia sifa zile ambazo huamini ni muhimu mwanaume wa kumuoa awe nazo. Vigezo hivyo huwa hata kwa misingi ya muonekano wa mwanaume huyo – kuna wale ambao hutaka mwanaume huyo wa kumuoa awe na sifa kama vile, mrefu, aliyejazia kifua, mtanashati, sauti nzuri n.k. Inaweza kuwa kama mzaha na ikaonekana ni kipengele kidogo sana lakini bado kuna wale ambao anaweza kuwa tayari kuolewa ila hataki sababu tu huyo mwanaume hafananii vile ambavyo yeye anataka mumewe awe.
Kutaka mwanaume tajiri
Kuna wanawake ambao tayari wameshajiwekea akilini kuwa hatakubali kuolewa na mwanaume yeyote yule ambaye hana pesa nyingi. Yupo tayari kuolewa ila si kwa mwanaume mwenye uwezo wa kawaida – hata ikitokea mwanaume ana uwezo kidogo wa kuweza kujitosheleza, yeye bado huona huyo mwanaume hamfai hadi pale tu atakapo pata yule ambaye anahisi ataishi maisha ya kifahari. Hivyo hukazana kusubiri na kujitahidi kuwinda aina ya mwanaume ambaye atakuwa na uwezo mkubwa, bila kujalisha kama huyo mwanaume kampita sana umri.
Kutompata Mwanaume Ampendae
Hili ni kama tu vile ilivyo kwa wanaume ambao huamini ndoa haiwezekani na haifai bali tu hadi pale umpatapo yule ambaye unampenda na unaamini anakupenda pia. Wengi katika kundi hili huamini kuwa mafanikio ya ndoa kigezo kikubwa ni kupendana tu na mengine hufuata kwenye sababu ya upendo. Kuna wanawake vigezo vya mwanamme awe vipi havina umuhimu kabisa katika kutaka kuamua kuolewa. Yeye kikubwa anataka ampate mume ambaye atampenda kwa dhati na huku akiwa na matumaini kuwa huyo mume atampenda na yeye pia kwa dhati. Huyu mwanamke anaamini msingi bora wa ndoa ni mapenzi ya dhati kati ya yeye na mmewe basi! Hana haraka hadi pale atakapompata mwanaume akampenda ndipo atakapokuwa tayari kuolewa.
Kuchagua mno Wanaume wa Kumuoa
Kuna wale wachache ambao akili hubadilika kama kinyonga; wasioridhika wala kujitambua ni nini wanataka ama mwanaume wa aina ipi wanataka. Akija wa mwenye uwezo atasema nataka wa kuchuma nae, akija asiye na uwezo atatoa sababu tu hata kama kumlaumu kuwa inaonyesha hajitumi kutafuta maendeleo. Akija wa kabila hii, atasema hapana hao wana tabia hii mimi siitaki! Yaani kwa ufupi ni mtu asiyeisha kutoa kasoro za wale ambao wanajitokeza kutaka kumuoa. Hatimaye inaweza tokea muda wa kuolewa ukapita na akaishia kupunguza uchunguzaji lakini ikiwa hata wanaume wa umri wa kufaa kumuoa kutokuwepo tena katika soko.
Kujiona ni mzuri sana
Kuna wanawake ambao ni kweli Mwenyezi Mungu kawajaalia uzuri hasa (uzuri wa muonekano), anakuwa ni mzuri kiasi kwamba wake kwa waume wote wanamkubali kwa uzuri huo na hata wote kumtamani. Hata hivyo hapo hapo kuna wale ambao huwa ni wazuri kawaida – ila kwa mtazamowake hujiona ni mzuri mno hakuna mfano kama yeye; kitendo ambacho kwa wachache kwenye kundi hili hufanya kujiona yeye ni yeye na kuwa kwa yeyote kuwa na yeye huyo mtu anatakiwa atambue kuwa ana bahati sana. Kitendo hiki hukuza nyodo za hali ya juu ya mwanamke mwenye mtazamo huu, kiasi kwamba wanapojitokeza wanaume kutaka kuoa – anaweza onyesha tabia kama maringo, dharau na kiburi.
Kujiona ana Umri mdogo
Binti yeyote wa miaka 18 na kuendelea anaruhusiwa kuolewa endapo tu karidhia kuolewa. Wanawake wametofautiana mipangilio yao ya kimaisha, kuna wale akiwa katika umri wa kuolewa hutamani sana kuolewa na kuna wale ambao hupenda kuolewa wakiwa wakubwa zaidi. Katika kundi hili umri kuwa mdogo hutegemeana, kuna mwingine anakuwa na umri wa miaka 25 na bado akajiona mdogo na hali kuna mwingine anakuwa na miaka 20 na akajiona ni mkubwa na anafaa kuolewa. Hii pia ni kwa wanawake wale ambao huwa na malengo ya kutotaka kuharakisha katika ndoa. Anapokuwa na umri ambao anaweza kuolewa lakini yeye hayupo tayari kwa muda huo, huwa ni kikwazo kwake kuingia katika ndoa.
Maradhi hasa UKIMWI
Hili kama lilivyo kwa wanaume – Pamoja na kuhamasishwa kwingi na wataalamu wa maradhi ya HIV/AIDS kuwa mtu hata ukiwa umeathirika unaweza kuwa na mahusiano na hata kuoa na kuwa na watoto; bado haisaidii sana kwa vijana wanaojitambua kuwa ni waathirika wakiwa bado ni wadogo, hawajaoa/olewa ama kuwahi kuwa na mtoto. Wengi sana hukata tamaa na huona ni kheri kubaki walivyo kuliko kuingia katika ndoa, hasa tokana na imani kuwa wanawake wakizaa wakati ni waathirika; afya hudhoofika zaidi.
Kutaka maisha ya Tamthilia (Ndoa za kuishi kwa furaha milele)
Kutokana na kukua kwa idadi ya tamthilia nyingi ambazo huonyesha maisha ya kimagharibi zaidi; kumekuwa na dhana kwa baadhi ya wanawake kutaka hayo maisha ya tamthilia yawe na kwao pia. Hilo linafanya vigezo ambavyo mwanamke huyo anatumia kuchagua ama kukubali mwanaume kumuoa kutotimiza yale ambayo yeye binafsi anatarajia. Wengi hushindwa kutambua kuwa hakuna maisha ya furaha milele, na hasa kuwa maisha ya maigizo yapaswa kuchanganya na zako kuweza kufanya maamuzi ya kipi kiigwe na kipi kiachwe kama kilivyo.
Kuona taasisi ya Ndoa kama Utumwa
Mtazamo huu kwa wanawake wenye msimamo huu, huchangiwa na baadhi kama haya:
– Usomi: Aina ya usomi ambao hupelekea kwa baadhi kuwa na tafsiri tofauti juu ya ndoa, haki, majukumu na mengine mengi.
– Kushuhudia ndoa mbovu: Hii inaweza kuwa ya wazazi/walezi wakewenyewe (pengine mama aliteswa sana), na hata ndugu wa karibu kama vile kushuhudia kila ndoa ya ndugu yake anayoijua mwanamke huishi kwa mateso, manyanyaso na maisha ya taabu na kuonewa.
– Kuwa na uwezo sana wa kujitosheleza ambao unaweza kumtimizia na kufanya lolote lile ambalo anataka katika maisha. Kwake kuwa na mwanaume kama mume kwake anaona kama ni utumwa.
Kutokuwa kabisa na mshipa wa hisia za kufanya mapenzi
Kuna wanawake wale wachache waliozaliwa hivyo. Hawana hisia yoyote ile ya kimwili ya kuweza kupata hisia za kuweza kujisikia ama kutamani kufanya mapenzi. Wengi wa aina hii ya wanawake huwa ni waoga sana wa kuwa karibu na mwanaume, na kwa wale ambao wamewahi hata jaribu baadhi huona kama kitendo cha ndoa ni kero, unyanyasaji na uchafu. Hivyo wazo la kuwa akiolewa anatarajia kufanya kitendo cha ndoa mara kwa mara kinamvunja kabisa hamu ya kutaka kuolewa.
Thursday, 30 July 2015
Matatizo ya Watanzania ni Makubwa Kuliko Vipimo vya GNP na GDP
Watu wa zamani kama kina Newton, Galileo, Faraday, na wa mwisho mwisho kama kina Einstein walikuwa wanafikiri sana. Na kufikiri kwao kumeleta mapinduzi katika jamii.Wapo pia Watu wa zamani kama kina Newton, Galileo, Faraday, na wa mwisho mwisho kama kina Einstein walikuwa wanafikiri sana. Na kufikiri kwao kumeleta mapinduzi katika jamii.
Wapo pia waliofanya hivyo katika Nyanja za uchumi na jamii. Leo tunatumia nadharia zao bila kufikiri wala kuhoji zaidi ili ikiwezekana tugundue au kuboresha nadharia zao ili zifae kutumika katika kizazi hiki. GNP, GDP n.k vililalia kwenye urahisi. Maisha ya watu huwezi kuyapima kwa rula. Mwanadamu ni mchanganyiko (complex) huwezi kuweka vipimo rahisi hivi kusema yuko na hali gani kijamii. Mfano Tanzania inasemwa kwa sasa hivi uchumi wake unakua kwa haraka na baadhi ya wanasiasa na watawala wanafurahi na kujitapa, lakini hali ya wananchi ikoje?
Tuesday, 21 July 2015
MAJAMBAZI WALIOVAMIA KITUO CHA POLISI CHA STAKISHARI, WAKAMATWA
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwa watuhumiwa wa ujambazi waliovamia kituo cha Polisi cha Stakishari, leo jijini Dar es Salaam.
Naibu wa Kamshina wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari juu operesheni iliyofanyika ya kuwakamata watuhumiwa wa ujambazi waliovyamia kituo cha Stakishari , jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Suleiman Kova akionyesha bunduki zilizoporwa katika uvamizi wa uliofanywa na majambazi katika kituo stakishari, leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Suleiman Kova akionyesha Fedha taslimu Sh.Milioni 170 zilizkutwa katika Shimo na majambazi waliovamia kituo stakishaari na kuua askari,leo jijiji Dar es Salaam.
Fedha za watuhumiwa ujambazi waliovamia kituo cha Polisi cha Stakiki zikiwa katika sanduku zikionyeshwa kwa waandishi habari na wananchi leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova akionyesha picha za amajambazi sugu wanaotafutwa na jeshi la polisi katika hafla ya kutuoa taarifa za kukamatwa kwa askari wa waliovamia kituo cha stakishari leo jijini Dar es salaam
Pikipiki zilizokuwa zikitumiwa na majambazi waliovyamia Kituo cha Stakishari zikiwa mbele ya Kamisha Kova wakati akitoa taarifa kukamtwa kwao leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka)
Na Chalila Kibuda.
MAJAMBAZI waliovamia Kituo cha Stakishari jijini Dar es Salaam watatu wauwawa na wawili watiwa mbaroni wakati wakitupiana risasi katika eneo la Tuangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo la kukamatwa na kuuawa kwa majambazi hao lilitokea Julai 17 mwaka huu huko maeneo ya Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam, majambazi hao walifanya tukio la kinyama la kuuwawa kwa askari wanne na raia watatu katika kituo cha Stakishari wanakadiriwa kuwa kati ya 16 hadi 18.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Suleiman Kova amesema kukamatwa kwa majambazi hao inatokana na kikosi kazi kilichoundwa na kanda maalumu kwa kushirikia na Mkoa Pwani.
Kukamatwa kwa watuhumiwa hao wa ujambazi kulitokana na taarifa pamoja na mtego wa kiintelejensia katika eneo la Tuangoma ndipo majambazi wakapita na pikipiki mbili walipowasimamisha askari majambazi hao walikaidi amri nakisha kuanza kurusha risasi na polisi wakajibu na majambazi watatu kuuwawa.
Majambazi waliouawa ni Abbas Hashimu Mkazi wa Mbagala, Yassin alitambulika kwa jina moja mkazi wa Kitunda Kivule, pamoja Saidi aliyetambulika kwa jina moja mkazi wa Mandimkongo, Mkuranga.
Kamanda Kova amesema wanaowashikiria ni Ramadhan Ulatule (15) ,Mkazi wa Mandimkongo, Mkuranga, Omary Amour( 24) Mkazi Mkazi wa Mbagala Kimbangulile.
Kova amesema baada ya kuwabana watuhumiwa wa ujambazi walikwenda kuonyesha bunduki 15 walizoporkatika a kituo cha Stakishari ambazo walikuwa wamehifadhi chini ya ardhi kuweka kinyesi juu.
Amesema katika Shimo walilohifadhi walikuta bunduki aina Norinko ambayo wanatafuta ilipoibiwa pamoja na kukuta fedha taslimu Sh.Milioni 170 za kitanzania.
Aidha amesema jeshi la polisi limejizatiti katika matukio na kutaka watu waachane na biashara hiyo ya ujambazi kuwa hailipi.
Amesema fedha hizo wanazichunguza kujua zimeibwa wapi, na pikipiki mbili aina ya boxer nazo wanazishiria na kutaka wauza pikipiki kuuzia watu ambao wanataarifa nazo.
“Hatutafumbia macho kwa wale askari wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu kwa kuwachukulia hatua kali ikiwa hata kama wanajihusiha na ujambazi tutawashughulikia kwani risasi haichagui kuwa huyu raia au askari”amesema Kamishina Kova.
Tukio la kuawawa kwa askari wanne na raia watatu katika kituo cha Stakishari,lilitokea julai 12 majira ya saa nne.
Subscribe to:
Posts (Atom)