Tuesday, 5 January 2016

TABIA MBAYA NA MBOVU KWA BAADHI YA WATU



Kwanza kabisa nianze kwa kusema kila mtu Duniani anaumuhimu wake na hakuna binadamu aliyekamilika chini ya hii ardhi au huu ulimwengu. Kwa kusema ivyo ni dhahiri kwamba kila mtu anamapungufu yake ambayo muda mwingine inakuwa ni kero au furaha kwa wengine.


Kuna katabia ambacho kameibuka miongoni mwa watu wengi hapa duniani sanasana katika hii nchi yetu yenye amani na utulivu. Unakuta watu wanapoishi na mtu eti kwa sababu tu ya hali yake duni kwa muda fulani au mapungufu fulanifulani basi wamekuwa wakimdharau nakumuona sio kitu kwao hata matendo na maneno yao wakati mwingine huonesha ubaguzi wa waziwazi.

Mapenzi ya Mungu ni Mengi na ndio maana kukawa nakausemi kwamba usimdharau mtu usiyemjua. Kauli hii wengi huitafsiria juu juu ila ukweli wake ni kwamba haitakiwi kumuonesha dharau mtu wa aina yeyote ile kwa sababu Hakuna mwenye ratiba ya binadamu mwenzake au anayeijua ratiba ya binadamu mwingine zaidi ya Muumba wa Mbingu na Nchi.

Nimalizie kukasema haka katabia ambacho kametokea kunichukiza sana maishani mwangu, unakuta watu wanaomsema mtu akiwa hai mara mzinzi mara mlevi mara mchawi kila siku wanatamka neno baya kwa huyo mtu mara mwizi mara changudoa mara muhuni wakutupwa mara sio mtu mzuri kila neno baya linatamkwa kwake hakuna neno zuri linalotamkwa kwake, siku mtu huyo akifariki au Mungu akimchukua Mbele za Haki watu walewale waliokuwa vieleele wakumtamkia maneno mabaya huanza kulia nakusema kwamba aliyekufa alikuwa ni mtu mwema na mwenye upendo na hakuna mtu mwenye upendo kama wake aliyewahi kutokea katika uso wa dunia hii.

Katabia haka kananiudhi sana kama hatutojibadilisha basi itakuwa ni tabu sana kutenda mapenzi ya Mungu chini ya Uso wa hii Dunia.


No comments:

Post a Comment