1. Fanya Kile Ukipendacho
Kuna mambo mengi hapa duniani ambayo ungeweza kuyafanya; kuna na mengine mengi zaidi ambayo ungeweza kujifunza na hatimaye kuyamudu kuyafanya. Kwa ufupi, una uwezo wa kufanya jambo lolote utakalo, endapo utajiamini na kuweka juhudi katika kutimiza jambo hilo.
Lakini sio kila jambo litakufaa wewe. Sio kila kazi utafurahia kuifanya. Sio kila kitu utakifurahia kukigusa. Kwa kuwa uwezo unao wa kufanya lolote utakalo, na kufanikiwa; hauna budi kuchagua jambo linalo furahisha moyo wako. Jambo litakalo kufanya uhisi kuwa unatoa mchango wa muhimu katika ulimwengu huu.
2. Weka Kipaumbele Katika Mahitaji ya Wengine
Hakuna kazi inayo faa, inayo pendeza, inayo furahisha na kuhamasisha kama kazi ya kutatua matatizo auhitlafu za watu wengine. Sio tu inakufanya wewe uwe mtu wa thamani katika maisha ya wengine, bali piainakupa fursa ya kupata kipato kutokana na juhudi hizo. Haijalishi ni jambo gani unalo lifanya, ilimradi linawasaidia wengine, lina faa sana.
Kuna kitu kimoja ambacho watu wote wenye kuwajali wengine wanafanania, UTAJIRI. Sio lazima uonekanokwa mfano wa mali nyingi; unaweza pia kuonekana katika uhusiano wako na watu wengine na kwa namna wengine wanavyo kuheshimu na kukuthamini. Dunia ina tawaliwa na watu wenye kuangalia mahitaji ya wengine kuliko yao, kuwa mmoja wapo.
3. Weka Bidii Kila Siku
Ghorofa halijengwi kwa siku moja, wala mafanikio kupatikana katika usiku mmoja. Usikate tamaa pale juhudi zako zinapo shindwa kuonekana na watu wengine, au msaada wako unapo shindwa kuthaminiwa na jamii. Badala yake, chukulia hii kama nafasi ya pekee ya kuboresha na kuongeza thamani ya kileunacho kifanya.
Kile unacho kifanya, kifanye kila siku. Unapo kifanya kila siku ndivyo kinavyo ongezeka thamani, ndivyokinavyo zidi kuwa chenye ubora, ndivyo watu wengi wanavyo zidi kukiona na kukijua na kukithamini. Unapofanya leo na kuacha kesho, hatimaye kukirudia kesho kutwa, kinapoteza ubora wake na kasi ya kufikia mafanikio unayo yakusudia.
4. Epuka Anasa Zisizo za Msingi
Sio kila hisia ni nzuri. Kicheko ni hisia nzuri lakini hasira ni hisia mbaya. Upendo ni hisia nzuri lakini chuki ni hisia mbaya. Vivyo hivyo katika swala la anasa au starehe. Kamwe, furaha yako usi-iegemeza kwenye starehe. Kama huna furaha na amani usitegemee utaikuta kwenye ulevi, uzinzi au madawa ya kulevya.
Furaha na amani ya kweli inapatikana katika mambo madogo-madogo yanayo tuzunguka kila siku. Kusaidiana, kushauriana, kutiana moyo, kutaniana, kucheza, kufanya kazi tunazo zipenda, kuimba, kutimiza wajibu wetu wa kila siku, kuwatembelea watu wenye madhaifu mbalimbali, kutembelea ndugu zetu wa mbalin.k. Na hizi ndizo anasa za msingi.
5. Shirikiana na Watu Wengine
Amin amin, katika ile ndoto yako unayo tamani kuitimiza, kuna mtu naye ana ndoto kama ya kwako. Kuna mtu ana ndoto ya kukusaidia wewe kufikia ndoto yako. Kuna mtu ana uwezo wa kukushauri, tena bure, ilikukuwezesha kufikia ndoto yako. Watafute watu hawa ushirikiane nao, uongee nao, uchangamane nao;watakusaidia.
Msaada wao sio tu utakusogeza mbele katika kufikia malengo yako, bali pia utakuunganisha nao na kuwafanya kuwa watu wa familia moja; wenye kutaka maendeleo. Pia utapata fursa ya kuonyesha upendo wako kwa kuwasaidia pale wanapo kwama au kushindwa; na kwa ishara hizi, amani na upendo na mafanikioyata kuzunguka siku zote.
6. Shukuru kwa Yote
Kuna wakati wewe unataka kukomba sahani na mtu anataka kukupa sahani iliyo jaa chakula. Na kwakutokujua kilichomo kwenye ile sahani mpya utaanza kulalamika, kulaani, kulaumu, kuhuzunika na kukosa amani. Kila jambo lina wakati wake, na hakuna linalo tokea pasipo ya makusudio; amini kuwa kuna faida katika kila jambo.
Kwa sababu leo hujafanikiwa haina maana kuwa hutafanikiwa kesho. Kwa sababu leo umekosa haina maana na kesho pia utakosa. Jifunze kusema ahsante. Jifunze kuridhika na kile ulicho nacho kwa wakati huo. Jifunze kushukuru hata kwa kile kidogo ulicho kipata. Kwa sababu ni kile kidogo kimoja kinacho unda kidogo kingine na hatimaye kikubwa.
No comments:
Post a Comment