Najua kila mmoja wetu kuna kipindi,anapatwa na hasira pale ambapo anaona ameendewa kinyume na alichotarajia.
Inawezekana ni ofisini,nyumbani, au hata njiani hali hii ikakukuta.
Je, kupatwa na hasira ni upungufu wa afya ya akili?
Jibu ni hapana,
hasira huwa zipo na zimeumbwa kwa kila binadamu.
Kwahiyo kushikwa na hasira ni jambo la kawaida ila kutenda jambo baya la kumdhuru mtu au mali kutokana na hasira huo ni upungufu.Kila mmoja wetu,anatakiwa awe makini katika kuzitawala hasira zake na aweze kujizuia pale anapoona zimezidi.Hebu tuangalie njia saba zinazoweza kukusaidia kuzitawala hasira zako:
1.ONDOKA ENEO HILO
Kama upo mazingira fulani na ukaudhiwa na hasira kali ikakushika,ondoka kwa dakika chache eneo hilo na ukafikirie vizuri.Ukifanya hivi,unasaidia kupunguza uzito wa yaliyokufanya uchukie kwani ubongo utapata nafasi ya kutafakari upya.
2.ELEZEA HASIRA YAKO UKIWA NA UTULIVU
Unapoelezea,hasira yako kwa mtu/watu waliokufanya ukasirike unasaidia kupunguza uzito wa tukio moyoni mwako.Elezea kwanini ulichukia na kwa utulivu kabisa bila kumuumiza mtu mwengine kwa maneno yako omba lisirudiwe tena.
3.FANYA MAZOEZI
Mazoezi ya viungo
yanasaidia kupunguza hisia kali
moyoni mwako pale
zinapotaka kuripuka.
Kama unaona una hasira nzito,
nenda eneo la mazoezi
anza kufanya mazoezi ya kukimbia au
kama una chumba cha mazoezi
kwako ingia anza kufanya mazoezi na utaona mabadiliko yake.
4.FIKIRIA KABLA HUJAZUNGUMZA
Ukiwa ushapamba moto wa hasira,
ni rahisi
kuzungumza maneno makali ambayo
yanaweza yakashusha utu wako au wa unayemwambia.
Chukua dakika chache,
kutafakari
maneno ya kutumia na uone kama hayatokuharibia au kumuharibia mwengine heshima yake.
5.FIKIRIA SULUHISHO MBADALA
Badala ya kuendelea kutafakari
kilichokufanya uchukie,
anza kufikiria namna ya kutatua tatizo lililojitokeza
kati yako na upande wa pili.
Yawezekana mtoto wako anaharibu vitu hovyo,
dereva wako anachelewa
kukufuata eneo unalomtaarifu,
au mpenzi wako anachelewa kufika eneo la miadi.
Fikiria suluhisho mbadala kwani tukio
baada hasira linaweza likaifanya
hali kuwa mbaya zaidi.
6.USILIMBIKIZE MATUKIO
Kusamehe matukio yaliyopita
na kuyasahau
ni njia inayopunguza uzito wa
tukio jipya.
Ukisamehe watu waliokukosea utakuwa umejisaidia mwenyewe na
wao pia kujifunza kitu kutokana
na tukio hilo.
Kwani usitarajie binadamu mwenzako awe
vile vile
unavyotaka na kutamani wewe awe.
7.TAFUTA MSAADA
Jinsi ya kuzuia
hasira ni
changamoto kwa kila binadamu,
kwani ukishindwa kuzizuia na
ukachukua uamuzi mbaya unawaumiza watu wanaokuzunguka.
Kwa hiyo chagua mtu wako ambaye utakuwa unaenda kuomba msaada wa ushauri
kutokana na
tukio lililokuudhi.
KUKASIRIKA SI DHAMBI
ILA INAONYESHA KUWA AKILI YAKO
INA AFYA YA KUJUA KIPI HUPENDI NA KIPI UNAPENDA KUFANYIWA.
LAKINI
UNATAKIWA UZITAWALE HASIRA
PALE UNAPOONA ZITAKUPELEKA KATIKA KUFANYA TUKIO BAYA DHIDI YA MWENGINE.
No comments:
Post a Comment